Puma yaibuka msambazaji mpya wa mipira EPL baada ya miaka 25 ya Nike



Kampuni ya vifaa vya michezo Puma ndiyo wasambazaji wapya wa mipira inayotumika kwenye Ligi Kuu England (EPL) kuanzia msimu huu, ikibadilisha rasmi nafasi iliyoshikiliwa na Nike kwa zaidi ya miaka 25.

Uamuzi huu umeleta upepo mpya katika ligi maarufu zaidi duniani, huku mpira mpya wa Puma ukitajwa kuwa na teknolojia ya kisasa inayoongeza kasi na mabadiliko ya ghafla hewani – jambo ambalo tayari limeanza kuonekana kama changamoto kubwa kwa makipa.


Kwa mujibu wa ripoti kutoka England, mpira huo mpya unaundwa kwa mfumo maalumu unaosaidia urahisi wa kupiga kwa usahihi na kuongeza nguvu za shuti. Wachezaji wengi wameonekana kufurahia, lakini upande wa makipa, mpira huo umeelezwa kuwa “tishio” kutokana na mabadiliko yake ya ghafla angani na kasi kubwa ya kuelekea langoni.

Hii ni mara ya kwanza tangu msimu wa 2000/01 ambapo ligi hiyo inatumia mpira usio wa Nike, hatua ambayo pia inatarajiwa kuimarisha ushindani wa kibiashara katika soko la vifaa vya michezo duniani.

Mashabiki wengi wanatarajia kuona namna mpira huu wa Puma utakavyoongeza msisimko wa mabao ya mbali na burudani zaidi kwenye viwanja vya EPL msimu huu.


"Habari hii imeletwa kwako na Habari 255"🇹🇿

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Tume ya Uchaguzi na NIDA Zakanusha Madai ya Humphrey Polepole

Mtanzania Afariki jangwani na mkenya kuvuka Boda