Trump: Kwa kuishambulia Iran, tulizuia 'vita' Mashariki ya Kati



Rais wa Marekani Donald Trump anasema iwapo Iran itarejelea mpango wake wa kurutubisha nyuklia, itashambuliwa tena na Marekani.

Bw.Trump, akijibu maswali ya wanahabari katika Ikulu ya White House siku ya Jumatano, alisisitiza kwamba Marekani imezuia vita katika eneo la Mashariki ya Kati kwa kuizuia Iran kupata silaha za nyuklia.

Kulingana na Bw. Trump, kabla ya Marekani kushambulia vituo vya nyuklia vya Iran vilivyo chini ya ardhi, nchi hiyo ilikuwa "miezi miwili tu kabla ya kupata silaha ya nyuklia."

"Tuliondoa uwezo wao wa kutengeneza silaha za nyuklia," Bw. Trump alisema, akiwa ameshikilia kielelezo cha bomu la B-52. "Iran ingeweza kuwa na silaha ya nyuklia ndani ya miezi miwili au chini ya hapo, lakini iliharibiwa kabisa."

"Tulizuia vita katika Mashariki ya Kati kwa kuzuia Iran kupata silaha ya nyuklia," Bw. Trump alisema. "Wanaweza kusema wataanza tena, lakini hiyo ni hatari kwao kwa sababu tutarudi."

Kulingana na Bw. Trump, "Iran ilikuwa nchi yenye chuki" na nchi "mbaya sana", na anadhani itakuwa tofauti katika siku zijazo



Araqchi: Hatuna makubaliano ya kujadiliana na Marekani

Sanjari na matamshi hayo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araqchi alihusisha mustakabali wa mazungumzo kati ya Tehran na Washington na "maslahi ya taifa."

Bwana Araghchi, akizungumza kwenye Idhaa ya 5 ya Jamhuri ya Kiislamu Jumatano usiku, alisema hakuna makubaliano ya uhakika ya kuanzisha tena mazungumzo ya nyuklia na Marekani.


Hadi sasa, duru tano za mazungumzo ya nyuklia yamefanyika kati ya Iran na Marekani, lakini mazungumzo hayo yalisitishwa kufuatia shambulio la Israel dhidi ya Iran.


Bw.Araqchi amesema katika hali ilivyo sasa kuna mabadilishano ya ujumbe baina ya pande hizo mbili.


Kulingana na yeye, muda na aina ya mazungumzo ya baadaye itategemea "maslahi ya kitaifa."


Bwana Araghchi pia alimwalika Naibu Mkurugenzi wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki kwenda Tehran kwa lengo la kujadili "mifumo mipya ya ushirikiano kati ya Iran na Shirika hilo.


Bw. Araghchi alisema: "Sasa Shirika linajua na Bw. Mkurugenzi Mkuu anapaswa kujua kwamba hali mpya kabisa imeundwa.


Tuna sheria zote mbili za bunge na hali ya msingi imebadilika. Vituo vyetu vingi vya nyuklia vimeshambuliwa na kulipuliwa na kuharibiwa."


Kulingana na Bw. Araqchi, kwa kuzingatia sheria mpya ya bunge, ushirikiano wowote mpya na Shirika hilo utahitaji idhini ya Baraza Kuu la Usalama la Kitaifa.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Puma yaibuka msambazaji mpya wa mipira EPL baada ya miaka 25 ya Nike

Tume ya Uchaguzi na NIDA Zakanusha Madai ya Humphrey Polepole

Mtanzania Afariki jangwani na mkenya kuvuka Boda