Chid Benz Arudi Mtaani Baada ya Miezi 10 ya Marekebisho

Msanii maarufu wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania, Chid Benz, amerudi mtaani baada ya kukaa kwa takribani miezi 10 kwenye nyumba ya marekebisho akipatiwa matibabu dhidi ya uraibu wa dawa za kulevya. Chid Benz, ambaye kwa muda mrefu alikumbwa na changamoto ya matumizi ya dawa za kulevya, amesema sasa yuko tayari kuanza ukurasa mpya wa maisha yake na amejipanga kulitumikia taifa kupitia kipaji chake cha muziki pamoja na kushirikiana na jamii katika mapambano dhidi ya dawa hizo. > "Nashukuru Mungu kwa kuniweka hai na kunipa nafasi ya pili. Nipo tayari kuonesha mfano bora na kusaidia vijana wenzangu kuepuka makosa niliyopitia," alisema Chid Benz. Mashabiki wake wengi wamepokea kwa furaha taarifa za kurejea kwake, wakimtakia kila la heri katika safari yake mpya ya maisha na sanaa. Wengi wanaamini kurejea kwa Chid Benz kutarudisha ladha ya Hip Hop ya Tanzania ambayo kwa muda imekuwa ikikosa sauti yake ya kipekee. "Habari hii imeletwa kwako na Habari 255"🇹🇿